Saturday, July 19, 2014

WAZIRI LAZARO NYALANDU AKUTANA NA BALOZI WA HESHIMA WA UTALII BEVERLEY, LOS ANGELES MAREKANI

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (kulia) akizungumza
na Balozi wa Heshima wa Utalii wa Tanzania nchini Marekani Bw. Ahmed
Issa juu ya mikakati mbalimbali ya kuvutia watalii wa kimarekani
kutembelea Tanzania jana Beverly, Los Angeles.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (kulia) akiagana na
Balozi wa Tanzania wa Heshima wa Utalii nchini Marekani Bw. Ahmed Issa
mara baada ya kumaliza mazungumzo juu ya masuala kadhaa ya kuvutia
Watalii wa Marekani nchini Tanzania jana Beverly, Los Angeles.

 
Mikakati inayotumiwa na Balozi wa Heshima wa Utalii wa Tanzania Bw.
Ahmed Issa kutangaza utalii ni pamoja na matumizi ya magari yenye
picha za vivutio vya utalii wa Tanzania katika majiji mbalimbali
katika California - Marekani kama inavyoonekana katika picha
 
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (kati) akiwa katika
picha ya pamoja na Balozi wa Heshima wa Utalii wa Tanzania nchini
Marekani Bw. Ahmed Issa (kushoto) na Bw. Abdul Majid baada ya kupokea
taarifa ya mikakati wanayoitumia kutangaza vivutio vya utalii wa
Tanzania kwa wamarekani jana Beverly, Los Angeles

No comments: