Shirika la Hifadhi za Taifa leo limekabidhi mchango wa Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kuendeleza sekta ya elimu mkoani Simiyu.
Mchango huo umekabidhiwa jana na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka.
Fedha hizi zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa shule maalum ya sekondari ya ufundi mkoani Simiyu ikiwa ni mojawapo ya mikakati ya mkoa katika kuimarisha sekta ya elimu ambapo pia mkoa umepanga kuje nga shule nyingine maalum mbili za sekondari za wasichana na wavulana.
Kwa pamoja Mhe Mtaka aliyeambatana na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga waliahidi kuzitumia fedha hizo kama zilivyokusudiwa na kuahidi kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha umuhimu wa wananchi kuheshimu sekta ya uhifadhi kwa kuwa ina manufaa makubwa kwao.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi aliahidi kuendelea kuwaunga mkono wana Simiyu kwa kuwa mkoa huo umekuwa mstari sa mbele katika kusimamia sheria za hifadhi hususan Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa kuzuia uingizaji wa mifugo pamoja na majangili.
Shule ya Ufundi ya Simiyu inatarajiwa kugharimu kiasi cha Shilingi Milioni 350 hadi itakapokamilika na wadau mbalimbali wameombwa kuunga mkono jitihada hizo za Simiyu.

No comments:
Post a Comment